Wednesday, January 7, 2015

Tottenham wamepewa nafasi ya kumchukua Saido Berahino na West Brom,, lakini kwa masharti ya kubadilishana na viungo Andros Townsend, 23, na Aaron Lennon, 27 (Daily Mirror), Leicester City wamewazidi kete Chelsea kwa kumsajili kipa kutoka Croatia Andrej Kramaric kwa mkataba wa pauni milioni 9.7 (Times), Real Madrid wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Norway Martin Odegaard, 16, ambaye anasakwa na timu nyingi za England. Man Utd wamesema hawajasikia lolote kutoka kwa mchezaji huyo aliyetembelea Old Trafford kabla ya Krismasi (Manchester Evening News), Arsenal bado wanataka kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, 25 (London Evening Standard), Arsenal pia watapambana na Southampton kutaka kumsajili kiungo kutoka Colombia Juan Quintero, 21 anayechezea Porto (Daily Star), beki wa Tottenham Younes Kaboul, 29, anajiandaa kuondoka baada ya kukosa 'namba' na Besitkas ya Uturuki inamnyatia (Sun), Liverpool imekubaliana na Bayern Munich kumsajili kiungo Xherdan Shaqiri, 23 kwa pauni milioni 10 (Daily Star), Arsenal wamekataa dau kutoka klabu ya Legia Warsaw ya Poland kumtaka kiungo Krystian Bielik (Sky Sports), Real Sociedad inayofundishwa na David Moyes ipo katika mazungumzo ya ngazi ya juu ya kumsajili kiungo wa Arsenal Joel Campbell, 22 (Mundo Deportivo), Borussia Dortmund itawaruhusu Manchester United kumsajili kiungo Ilkay Gundogan, 24 (Daily Express), West Ham wameonesha nia ya kumtaka kiungo wa Atletico Madrid Mario Suarez (Daily Mail), Liverpool bado hawajazungumza na Lille kutazama uwezekano wa kumrejesha Divock Origi (TalkSport), mshambuliaji wa Chelsea Islam Feruz, 19, anataka kujiunga na Cardiff City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu (Wales Online), Na katika habari nyingine mshambuliaji wa Manchester City Sergio 'Kun' Aguero, 26, huenda akarejea uwanjani katika mechi dhidi ya Everton siku ya Jumamosi baada ya kumia goti (Manchester Evening News), kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 24, anatarajiwa kucheza mechi dhidi ya Stoke City siku ya Jumapili, licha ya mtafaruku wa kuvuta sigara bafuni siku ya mwaka mpya (Guardian). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Habari za usajili zilizothibitishwa nitakuletea pindi nitakapozipata. Cheers!!

Source: Salim Kikeke

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video