Tuesday, January 27, 2015

Mshambuliaji kutoka Brazil Douglas Costa, 24 ameiomba klabu yake ya Shakhtar Donetsk kutomuwekea bei kubwa ili kuzuia asiende Chelsea mwezi huu (Daily Mirror), Chelsea na Manchester United wamepata matumaini baada ya boss wa Juventus Massimiliano Alegri kusema itakuwa vigumu kukataa dau la pauni milioni 75 kwa kiungo Paul Pogba (Metro), wakati huohuo juhudi za Man Utd kumfuatilia Kevin Strootman, 24 huenda zikatapa pigo baada ya mchezaji huyo wa Roma kupata jeraha la goti katika mchezo dhidi ya Fiorentina (Sun), wakala wa winga Adnan Januzaj, 19 amesema kuwa meneja wa Man Utd Louis van Gaal amezuia hatua yake ya kwenda Paris St-Germain au timu nyingine (Telegraph), Southampton wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka Uholanzi Jordy Clasie, 23 kutoka Feyenoord (Daily Mirror), Andre Schurrle, 24 huenda asicheze mechi ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool, kwa kuwa Wolfsburg wanajaribu kukamilisha uhamisho wake (Telegraph), meneja wa Arsenal Arsene Wenger anafikiria kumfuatilia beki wa kulia wa Valencia Joao Pereira na beki wa kati wa AC Milan Adil Rami (Daily Star), Arsenal pia wanajaribu kumchukua Kevin Grosskreutz kutoka Borussia Dortmund baada ya kumchukua Gabriel Paulista (Daily Express), Liverpool inataka kumchukua mshambuliaji wa Arsenal Chuba Apkom, 19 ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu (Daily Star), Stoke City wanakaribia kuwasajili Adama Traore na Sandro kwa mkopo kutoka Barcelona hadi mwisho wa msimu (Daily Star), beki wa kati wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte atakubali kuhamia Old Trafford ingawa Man Utd hawajatangaza dau lolote (Sky Sports), Liverpool wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Manchester City James Milner mwisho wa msimu (ESPN) Tetesi nyingie kesho tukijaaliwa. Cheers!

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video