Meneja wa West Brom Tony Pulis ametoa dau la pauni milioni 4 kumtaka winga wa Wigan Callum McManaman, 23 ingawa Wigan wanataka pauni milioni 6 (Daily Telegraph), Swansea nao wametoa dau la pauni milioni 4 kutaka kumsajili beki Martin Olsson (Daily Express), Manchester United wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 25 kwa pauni milioni 40, pamoja na kipa David De Gea, 24 ambaye thamani yake ni pauni milioni 40 (Manchester Evening News)
Liverpool imebadili nia yake ya kumrejesha Divock Origi, 19, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 10 na kurejeshwa Lille kwa mkopo (Daily Star), Liverpool wapo katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Ispwich Teddy Bishop, 18 (Daily Mirror), beki wa kati wa Villarreal Gabriel Paulista, 24 amesema wakala wake yupo katika mazungumzo na Arsenal juu ya uhamisho mwezi wa Januari (Sky Sports). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Usajili uliothibitishwa, nitakujulisha utakapothibitishwa.
0 comments:
Post a Comment