Bayern Munich wameacha na mpango wa kumsajili Marco Reus
Bayern Munich wameachana na mbio za kumsajili Marco Reus na kuacha milango wazi kwa klabu ya Real Madrid na klabu kubwa za ligi kuu England.
Bayern wamefikia maamuzi ya kutomshawishi Reus wiki kadhaa zilizopita kwa madai kuwa tayari wana viungo washambuliaji wengi na hawataki kuharibu uhusiano wao wa karibu na Borussia Dortmund, hii ni kwa mujibu wa gazeti la Bild.
Real wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Reus, lakini kutokana na tetesi za klabu za Hispania kufungiwa usajili, anaweza kutua katika timu za ligi kuu England majira ya kiangazi mwaka huu.
Reus ni miongoni mwa wachezaji wakubwa barani ulaya na atazivutia klabu kubwa.
Taarifa za Bayern kutomsajili zitawashitua Manchester City na Chelsea ambao wanaendelea kutumia pesa kuimarisha vikosi vyao ili kufikia ubora mkubwa wa ulaya.
0 comments:
Post a Comment