EMMANUEL Okwi kamili gado kuivaa JKT Ruvu Stars
katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara, kwa mujibu wa taarifa za uhakika
kutoka kambi ya Simba iliyopo Hoteli ya Ndege Beach, kambi ya Jeshi Mbweni,
jijini Dar es salaam.
Mganda huyo kipenzi cha Wanamsimbazi jana alifanya
mazoezi kikamilifu chini ya kocha mkuu Goran Kopunovic na Mserbia huyo alisema
anaendelea vizuri na anamtumia kwenye mechi ya leo.
Okwi aliumia Januari 24 katika sare ya 1-1 baina
ya Simba na Azam fc uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Beki wa kati wa Azam, Aggrey Morris alimpiga
kiwiko na kuzimia uwanjani, lakini sasa yuko fiti kabisa.
Habari njema zaidi kwa Mashabiki wa Simba, beki
mahiri wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy naye anacheza leo kwa asilimia zote.
Kessy hakuwepo kwenye kikosi cha Simba
kilichofungwa 2-1 na Mbeya City fc jumatano iliyopita.
Hata hivyo, Said Hamis Ndemla ataendelea kukaa nje
kutokana na majeruhi.
Taarifa za asubuhi hii kutoka kambi ya Simba
zinaeleza kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri, kocha amefanya nao kikao na
sasa wamerejea katika saikolojia nzuri tayari kuwavaa JKT Ruvu.
Wakati huo huo Rais wa Simba, Evans Aveva alikiri
jana kuwa kufanya vibaya kwa Simba ni kutokana na uchovu wa wachezaji.
Simba walitoka kombe la Mapinduzi ambako walicheza
mechi sita mfulilizo na walirudi bara na kwenda moja kwa moja Mtwara
walikoshinda mabao 2-0 dhidi ya Ndanda, wakarudi Dar es salaam na kutoka sare
ya 1-1 na Azam fc na kufungwa na Mbeya City katikati ya wiki hii.
0 comments:
Post a Comment