Thursday, January 22, 2015


Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij (kushoto) ameshindwa kuifunga Rwanda

Na Bertha Lumala
Baada ya kufungwa katika mechi mbili zilizopita, kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimezinduka na kuilazimisha sare ya bao moja timu ya taifa ya Rwanda 'Amavubi' katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo jioni.

Kikosi cha Amavubi cha leo kimeanza na kiungo mahiri wa Yanga, Haruna Niyonzima lakini kimebanwa vilivyo na makinda wa Tanzania wanaoandaliwa kwa ajili ya michuano ya baadaye ya kimataifa.

Stars Maboresho iliyoanzishwa baada ya kuingia madarakani kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi mwaka juzi,  ilifungwa na Burundi katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki zilizopita.

Ilianza kufungwa mabao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyoandaliwa kwa ajili ya kuazimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, mwaka jana.

Timu hiyo ikiwa chini ya Mholanzi Mart Nooij, ilifungwa pia mabao 2-1 dhidi ya timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ya Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kuadhimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara Desemba 9, mwaka jana.

Katika mechi ya leo, wageni wamekuwa wa kwanza kutikisa nyavu baada ya Mugereza Batist kujitwisha kichwa mpira wa krosi ya wingi ya wingi ya kulia, mpira ambao ulimshinda kipa kinda wa Simba, Peter Manyika Jr dakika ya 14.

Winga kinda wa Azam FC, Kelvin Friday ameisawazishia Stars kwa shuti kali dakika moja kabla ya mapumziko, matokeo ambayo yamedumu hadi dakika ya mwisho ya mechi hiyo licha ya timu zote kufanya mabadiliko kadhaa.

Baada ya mechi hiyo kumalizika, Salum Mayanga, kocha msaidizi wa Taifa Stars, amesema benchi lao la ufundi limeridhishwa na namna timu ilivyochezwa dhidi ya timu iliyokaa pamoja kwa muda mrefu ya Rwanda.

"Ni matokeo mazuri kwetu ingawa tunachokiangalia katika kikosi chetu si matokeo, bali ufundi utakaotusaidia kupata timu nzuri kwa ajili ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan)," amesema Myanga.


Vikosi vya Stars na Amavubi vya leo vilikuwa:
Taifa Stars Maboresho: Manyika Peter, Miraj Adam, Gadriel Michael, Andrew Vicent, Joram Mgeveke, Salum Mbonde, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Kelvin Friday, Simon Msuva na Shiza Ramadhan/ Salum Telela (dk 45).

Rwanda: Olvier Kwizera, Baysega Emiry, Ismail Nsutyamagara, Sekamana Mayime, Rusheshanganga Michael, Mugereneza Batist, Haruna Niyonzima, Bigirimana Issa, Sibomana Patric, Mutuma Janveer na Iradukunda Betrand.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video