Friday, January 16, 2015

MGANDA Simon Sserunkuma na Mzawa Said Hamis Ndemla wapo tayari kuivaa Ndanda fc katika mechi ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara itakayopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio ameuambia mtandao huu dakika chache zilizopita kuwa Simon aliyeumia kwenye mechi ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Polisi na kuukosa mchezo wa fainali na Mtibwa Sugar ambapo Simba ilishinda kwa penalti 4-3 na kutwaa kombe jana alifanya mazoezi kwa asilimia 100.

Pia Ndemla aliyeumia kwenye mechi ya fainali ya Mapinduzi januari 13 mwaka huu yuko kamili gado kuwavaa Ndanda wenye usongo wa kupata pointi tatu muhimu.

“Wachezaji wote wazima, Simon na Ndemla wako safi kabisa, hakuna tatizo. Jana tumefanya mazoezi na leo jioni tunaenda kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi ya kesho”. Alisema Nyasio.

Kikosi cha Ndanda fc

Simba wenye morali kubwa baada ya kutwaa taji la Mapinduzi wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar desemba 26 mwaka jana na kipigo hicho kilimfukuzisha kazi kocha mkuu Patrick Phiri.
Kocha mpya Goran Kopunovic baada ya kufanya kazi nzuri Zanzibar ataiongoza Simba kwa mara ya kwanza katika mechi ya ligi kuu.


 Katika mechi 8 za kwanza, Simba ilitoa sare sita, ikashinda moja na kufungwa moja.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video