Tuesday, January 6, 2015

Simba na Yanga ndio baba wa soka la Tanzanaia

Katika maisha kipimo kizuri cha kutambua wewe ni nani haswa ni kile cha kujua nini unafanya na nini  umepata au unamiliki.  
Hii ni kauli ya Vince Lombardi  akiwa ni moja ya makocha wa kukumbukwa na kuheshimika sana katika ligi ya Mpira wa marekani (NFL) maarufu kama American Football.    Wala hakua mbali na ukweli alikuwa sahihi sana,  unapata vipi shida kujilinganisha na jirani yako wakati unajua fika kipi unafanya na kipi unamiliki? 
 Hii ndio akili yetu Watanzania hapa ndipo tunapokwama, tunapenda kujilinganisha na jirani bahati mbaya sana akapiga hatua kadhaa mbele tunamsahau na kumtafuta jirani mwingine ambaye tunahisi tunakaribiana naye kiuwezo huku tunasahau kuboresha ubora wa kile tunachofanya ili kuongeza pia tunachomiliki.  
Tumekwama hapa katika kila kitu,  kisiasa,  uchumi,  biashara na hata michezo.  Unajua riadha tunajivunia nini?  Mpira wa Pete je (netiboli),  mpira wa kikapu? Achilia mbali alipofika Hasheem Thabeet lakini bado na yeye yupo hapa.  Alitakiwa awe mbali sana.  Yaache hayo tizama mchezo pendwa wa soka. Ushajiuliza mchezaji yupi wa kizazi cha sasa atawahi kufika kucheza soka la kulipwa Ubelgiji achilia mbali Uingereza na majirani zake?  Kiuhalisia unaona hayupo hata wachezaji wenyewe wanaamini hayupo. Ndoto zao kufika alipo Samata kwanza wala hawamuwazi tena Jirani Yao Wanyama, Mayuka,  yule Mariga ndio walishamsahau. Wengi wanaamini kama isingekuwa kubahatika kukutana na Mazembe klabu bingwa Samata angekuwepo Simba. Watanzania tunaishi na neno bahati mioyoni na akilini.
Leo ni mwaka 2015, takribani miaka mitatu ama zaidi tangu Ramadhani Singano,  Simon Msuva,  Salum Telela na akina Jonas Mkude,  Shomari Kapombe waitwe makinda. Hawapo kundi Hilo tena. 
Sasa wakiwa ni moja ya wachezaji tegemewa kuunda kikosi cha taifa. Hawa Hawa wametoka kusaini mikataba mipya. Hiki ndicho kizazi ambacho tunatakiwa tukitegemee mwaka 2018 na pengine 2022. Unazijua ndoto zao?  Moja yake ishakamilika katoka Ufaransa karudi Azam,  mwingine kasaini na pesa kapewa wengine wanaelekea katika mkondo huo huo.  Hata wanaokuja wataishi maisha haya haya. Lakini je ni kweli soka la kimaitafa limetulaani kiasi hiki?  

Ni kweli hatuwezi kucheza soka Ufaransa vyema au Ubelgiji sehemu ambayo wengi huanzia maisha ya soka haswa kwa waafrika.  Unaupenda umahiri wa Yaya Toure, unatamani kufika alipo, unazijua njia alizopitia?  Jirani yako Wanyama unajua hatua alizoanzia?  Unaiwaza Westham kabla ya Celtic,  Unaiwaza Barcelona kabla ya Anderletch Kisha yakishindikana unakuja na wazo moja tu la haiwezekani.  Watanzania tunaishi hivi.  

Wachezaji wameamua kuishi hivi,  viongozi wa soka wanatupeleka tuishi hivi,  wapenzi wa mpira tunaamini hivi. Kuwa kufanikiwa ni bahati, isipokuwepo bahati ni haiwezekani. Uongo Ulioje.  Ligi ya Brazil ni kubwa maradufu kuliko ya Tanzania lakini maelfu wanauza mboga wapate viatu vya soka.
 Wanaamini katika kujituma na sio bahati. Hapo ndipo unapata mchezaji bora wa kariba ya Alexis Sanchez.  Hapo ndipo unamtoa Yaya Toure.  

Sio katika kusubiri bahati kama ninavyomtizama Msuva akiisubiri Yanga au Haruna Moshi alivoiacha.  Maisha yanawastahili wale waliyoyaandaa.  Ndo maana mwandishi maarufu marekani Peter F Drucker aliwahi kusema "kama ukiona biashara au shughuli iliyofanikiwa basi ujue Kuna mtu alifanya maamuzi yaliyohitaji ujasiri"
Nilikuwa nauwaza umri wa Mbwana Samata.  Nikiwa nadhani ni moja ya wachezaji wa kitanzania wenye nafasi ya kufika mbali lakini naona ni ndoto nilizonazo mwenyewe kichwani. Naona haitokei.
  Yupo nyuma ya muda ukizingatia namna wengine waliofanikiwa walikopitia. Labda itokee bahati sana kama wengi tunavyopenda kuamini. 
Thomas Ulimwengu,  huyu nilianza kumsahau huko tangu aliporudi kutoka Ujerumani. Imenibidi nikikumbuke kile kizazi cha Copa Coca-Cola kilichofanya makubwa Brazil mwaka 2007 hivi kimeishia wapi?  Jerome Lambele, Moka Shabani,  Faraji,  Mohamed golikipa aliyesifiwa sana hata na makocha wa Brazil,  nadhani Himid Mao ndiye aliyesogea mbele kati yao. 
Kile kituo cha soka je kilichokuwa chini ya TFF nacho kilikufa,  nakitizama kituo cha Alliance Mwanza wana mlengo mzuri kwa vijana bahati mbaya sana umelenga pasi na kutarajia huku kwa mapacha Simba na Yanga. Vijana ndio soka la sasa,  lakini watanzania kwa ujumla hatujui hilo. Mawazo yetu makubwa ni kutorokea uarabuni mikataba ikigoma. 
Tunalipenda kweli neno haiwezekani.  Yule Rais wa UFARANSA NAPOLEON BONAPARTE alikuwa haamini katika neno HAIWEZEKANI. Aliamini hili neno halipo. Kwake hili neno lilikuwa linapatikana kwenye kamusi ya wajinga. Tangu ametamka ni miongo imepita sasa, lakini roho inaniuma nikihisi alitusema sisi pasipo kujua.  Umeiona sura ya Ngasa sasa hivi Yanga.  
Anajua kabisa hana maisha marefu pale kwa kosa alilofanya misimu miwili ilopita. Alisahau mwili hauna rafiki, kiwango hakina ndugu.  Hata hivyo naye aliikumbatia kamusi hii tuloikumbatia Watanzania wengi. Kamusi ya mjinga.

 Ndo maana tunaamini soka la kulipwa kwetu haiwezekani,  si haba hata Haruna Moshi alitutangulia kuamini hivyo.
Ahsanteni 
By Nicasius Coutinho Suso

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video