Tuesday, January 20, 2015


Simba SC wamepania kufuta uteja kwa Azam FC? Baada ya kufungwa katika mechi zote mbili za msimu uliopita, wekundu hao wa Msimbazi wanatarajia kuingia kambini Ndege Beach, Dar es Salaam kesho Jumatano kunoa makali kabla ya kuwavaa mabingwa watetezi Azam FC.


Simba SC iliyotwaa taji la tatu la michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari 13 kisha kuilaza kwa mabao 2-0 Ndanda FC mjini Mtwara mwishoni mwa wiki, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Azam FC katika mechi yao ya raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.

Msemaji wa Simba SC, Humphrey Nyasio amesema: "Wachezaji walipewa mapumziko baada ya mechi yetu dhidi ya Ndanda FC. Jumatano tutaingia kambini Ndege Beach tayari kwa mazoezi maalum kwa ajili ya mechi inayofuata dhidi ya Azam FC."

Wakati Simba SC wanaanika mipango yao hiyo, wapinzani wao Azam FC wako Kanda ya Ziwa na kesho jioni kikosi hicho cha Mcameroon Joseph Omog kitashuka Uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Kagera Sugar katika mechi yao ya kiporo ya raundi ya 10 ya VPL.  

Azam FC, Mtibwa Sugar FC, Simba SC na Yanga SC hazikuchyeza mecbi zake za raundi ya tisa na 10 ya VPL msimu kutokana na uwapo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Azam FC, mabingwa watetezi wa VPL, hawakufungwa na Simba SC katika mechi mbili zilizopita wakiifunga 2-1 katika mechi zote za msimu uliopita.

Simba SC inajivunia usajili wake wa dirisha dogo kwa kunasa saini za wakali watatu kutoka Uganda, Simon Sserunkuma, Juuko Murushid na Dan Sserunkuma, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) msimu uliopita ambaye Jumamosi alifungua mlango wa mabao Simba kwa kufunga bao katika ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC baada ya kucheza mechi nane bila goli.

Wanalambalamba, Azam FC wanatamba na kurejea kwa kinara wa mabao Mrundi Didier Kavumbagu, mapacha kutoka Ivory Coast Michael Bolou na Kipre Tchetche waliokuwa wagonjwa pamoja na kiungo mzawa Frank Domayo ambaye Jumamosi alicheza mechi yake ya kwanza VPL akiwa na Azam FC na kufunga bao katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.

Azam iko nafasi ya pili katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 17 sawa na vinara Mtibwa Sugar, tatu mbele ya Kagera Sugar iliyoko nafasi ya sita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video