Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba imewanyima pointi tatu
muhimu mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Azam fc almaarufu kama
wanalambalamba katika mchezo wa kuwania ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa
leo hii katika dimba la uwanja wa taifa jijini Dar e s salaam.
Emmanuel Okwi akijaribu kumtoka kumtoka Beki wa pembeni wa azam Shomari kapombe
ilikuwa ni simba iliyopata bao la kuongoza kwa kupitia mshambuliaji raia wa kiganda Emmanuel okwi goli lililodumu
mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, lakini kipindi cha pili Azam ilicharuka
na kuliandama lango la wekundu wa msimbazi Simba,
wachezaji wa Azam wakishangilia goli la Kipre Tcheche kutoka kushoto Kipre Tcheche,John Boko, khamis mcha.
na katika dakika ya hamsini
na saba mshambuliaji Raia ya Ivory Coast Kipre Tcheche aliweza kusawazishia Azam
na kupelekea timu hizo kugawana pointi moja moja, huku azam bado ikiwa
inashikilia usukani wa ligi kwa kujikusanyia pointi 21 na simba ikifikisha
pointi 13.
na Frank Momanyi
0 comments:
Post a Comment