Baada Ndanda fc sasa zamu ya Azam fc
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanaanza mazoezi kesho
asubuhi kuitafutia dawa Azam fc wakayopambana nayo katika mechi ya ligi kuu soka
Tanzania bara itayofanyika uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Meneja wa Simba, Nico Nyagawa ameuambia mtandao
huu asubuhi hii kuwa kocha Goran Kopunovic
alitoa mapumziko kuanzia jana jioni na leo baada ya ushindi wa mabao 2-0
waliopata jumamosi iliyopita dhidi ya Ndanda fc kwenye uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mkoani Mtwara.
“Tunaanza mazoezi kesho asubuhi, lakini bado
hatujathibitisha uwanja tutakaotumia, kufikia baadaye mchana nitatoa taarifa
niwapi tutakuwa na program”. Amesema Nyagawa.
Mechi hiyo ya wikiendi itakuwa ya pili katika ligi
kwa kocha Kopunovic ambaye mpaka sasa hajafungwa mechi yoyote tangu aanze kazi
ya kuifundisha Simba katika michuano ya kombe la Mapinduzi na alifanikiwa
kutwaa kombe hilo januari 13 mwaka huu kwa kuifunga Mtibwa Sugar penalti 4-3
katika mechi ya fainali.
0 comments:
Post a Comment