Saturday, January 17, 2015

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Ndanda fc katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona.
Simba waliandika bao la kuongoza katika dakika ya 32 na Danny Sserunkuma akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Elius Maguri.

Simba walienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili, Mnyama aliendelea kushambulia na katika dakika ya 52 waliandika bao la pili kupitia kwa Elius Maguri aliyemalizia kazi nzuri ya Danny Sserunkuma.


Hili ni goli la kwanza kwa Danny katika mechi 9 alizoichezea Simba kwa maana ya ligi, Nani Mtani Jembe na kombe la Mapinduzi.
Huo ni ushindi wa kwanza katika mechi ya kwanza ya ligi kwa kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic.


Goran ameendeleza ushindi kutokea kombe la Mapinduzi ambako alitwaa kombe hilo januari 13 mwaka huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video