Sunday, January 4, 2015


Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman amemaliza gundu la ukame wa mabao katika kikosi hicho cha Jangwani baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 walioupata dhidi ya Taifa ya Jang'ombe.

Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar juzi ilikuwa ya Kundi A la michuano ya Kombe la Mapinduzi. 

Sherman ambaye alikuwa hajafunga bao tangu ajiunge na Yanga SC dirisha dogp, alifunga bao hilo akimalizia krosi ya winga hatari Simon Msuva ambaye alifunga mabao yote matatu ya mwanzo na kuondoka na mpira wa zawadi ya 'hat-trick'.

Baada ya mechi hiyo, Sherman alisema: "Ninajisikia vizuri kwa kufunga bao langu la kwanza katika maisha yangu ndani ya timu mpya ya Yanga. Ninatarajia mambo mazuri yanakuja."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video