Wednesday, January 7, 2015

Kikosi kilekile kilichoanza dhidi ya JKU kinaanza leo

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MGANDA Saimon Sserunkuma ambaye hukuwepo katika mechi tatu za makundi za kombe la Mapinduzi leo majira ya saa 2:15 usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar mjini hapa anaanzia benchi Simba SC ikipepetana na Taifa ya Jang’ombe kwenye kipute cha kwanza cha Robo fainali ya kombe hilo.

Kocha mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic amemuanzisha langoni Manyika Peter, wakati beki wa kulia anaanza Hassan Ramadhani Kessy na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ anaanza mbavu ya kushoto.

Mabeki wa kati ni Juuko Mursheed na Hassan Suleiman Isihaka.

Kiungo wa ulinzi anaaza Jonas Gerard Mkude , kiungo namba nane anaanza Said Ndemla, wakati winga ya kulia anaanza mfungaji wa goli lililoivusha Simba Robo fainali dhidi ya JKU, Ramadhani Singano ‘Messi’.

Winga ya kushoto ataanza Awadh Issa Juma na mshambuliaji wa kati anasimama Elius Maguli na nyuma yake (kiungo mshambuliaji namba 10) anaaza Danny Sserunkuma.

Wachezaji wa akiba ni Denis Richard, Nassor Masoud, Issa Rashid, Abdallah Seseme, Ibrahim Ajib, Ibrahim Twaha, Shaban Kisiga, Simon Sserunkuma na Abdi Banda.

Kopunovic ataanza na mfumo wa 4-2-2 ambao unatumiwa zaidi na Mnyama Simba.

Kikosi  cha kwanza hakina mabadiliko, wachezaji wote walianza katika mechi ya mwisho ya makundi Simba ikishinda bao 1-0 dhidi ya Vinara wa Zanzibar, JKU.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video