Friday, January 23, 2015


Arsenal manager Arsene Wenger wants work permits for foreign footballers to be scrapped
 Wenger anataka vibali vya kazi kwa wachezaji wa kigeni vifutwe 

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anataka vibali vya kazi kwa wachezaji wa kigeni vifutwe.
Mfaransa huyo ambaye amekiri kwamba alishindwa kumsajili Angel di Maria klabuni hapo miaka 9 iliyopita kwasababu ya kukosa kibali cha ajira.
Amesema mamlaka za soka za UK zifungue mipaka kwa wachezaji wote duniani, na sio lazima kwa wale tu wanaokidhi vigezo vya kupata vibali vya kazi kama ilivyosasa.
Arsenal wamesimama kumsaini beki wa Villarreal, Gabriel Paulista ambaye ada yake ni paundi milioni 15.
Usajili wa beki huyo raia wa Brazil umesimama kwasababu ya kibali cha kazi na haitakuwa rahisi kwasababu beki huyo wa kati hajawahi kucheza soka la kimataifa.
Villarreal's Gabriel Paulista (right) could be heading for Arsenal if they can secure a work permit
 Gabriel Paulista (kulia) anaweza kujiunga na Arsenal kama wataweza kupata kibali cha kazi 

Kanuni inasema kuwa wachezaji ambao wamecheza asilimia 75 ya mechi za mataifa yao ndani ya nchi 70 za juu kisoka katika miaka miwili iliyopita ndio wanastahili tu kupata vibali vya kazi.
Hii inawanyima haki wachezaji wa akademi kujiunga na timu za kwanza. Arsenal wanasema kama watashindwa kumsajili Paulista mwezi huu watakata rufaa.
Msimu ujao kutakuwa na kanuni mpya inayosema wachezaji wenye thamani ya paundi milioni 10 watapewa vibali vya kazi. Lakini Wenger anasema sheria ya vibali vya kazi inatakiwa kufutwa akidai inaweza kusaidia kupata wachezaji vijana waliokamilika.
"Lengo la ligi kuu England ni kuwa ligi bora duniani,' Amesema Wenger. "Kwahiyo lazima uweke wazi mipaka.
"Tulimvumbua Di Maria alipokuwa na miaka 17. Tulihitaji aje hapa, lakini alienda Ureno, kutoka Ureno akaenda Hispania. Kwanini? Kwasababu asingeweza kupata kibali cha kazi hapa. Hii inamaanisha unaweza kumpata England wakati ana thamani kubwa ya fedha".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video