Monday, January 26, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Klabu ya Simba italimwa faini na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kutopeleka timu uwanjani wakati wa mechi yao iliyopita dhidi ya Azam FC.

Simba haikupeleka kikosi B kumenyana na kikosi B cha Azam FC kabla ya kuanza kwa mechi yao ya raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Humphrey Nyasio, msemaji wa Simba, ameuambia mtandao huu jijini hapa kuwa wamefanya kosa hilo kutokana na "matatizo ya ndani ya uongozi wa klabu."

"Hatukupeleka timu yetu ya vijana uwanjani jana kwa sababu haikufanya mazoezi wiki iliyopita kutokana na matatizo ya ndani ya uongozi ambayo sijapewa ruhusa ya kuyazungumzia kwa sasa," Nyasio amesema na kuongeza:

"Kuna kikao kinaendelea Rais (Evans Aveva) amekutana na Kamati ya Ufundi, Ninafikiri kesho tutakutana na waandishi wa habari kuelezea kwa kina suala hilo."

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, zinadai kuwa wachezaji wa Simba B wamegoma kufanya mazoezi kutokana na kutolipwa posho.

Simba itapigwa faini ya Sh. 500,000 na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kwa kutopeleka kikosi B uwanjani, kwa mujibu wa Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2014.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video