Baada ya
kufunga goli mbili juzi, Nyota na mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014, Cristiano
Ronaldo ameefanikiwa kumpiku Carlos Alonso Santillana na hatimaye kuwa wa tatu
katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu hiyo kunako michuano
mbalimbali. Ronaldo amefikisha magoli 289 akimwacha Santillana mwenye 288.
katika idadi hiyo mabao 206 ameyafunga katika ligi, mabao 21 kunako kombe la
mfalme, mabaoo 57 katika michuano ya klabu bingwa ulaya, mawili michuano baina
ya bingwa wa UEFA kubwa na ndogo na mengine matatu katika pambano la ufunguzi
wa ligi ya Hispania.
na kwa maana hiyo sasa, Ronaldo, almaarufu CR7 amebakiza magwiji wawili pekee
ambao ni Alfredo Di Stéfano mwenye 307 na mhispaniola Raúl González, mwenye 323.
0 comments:
Post a Comment