Monday, January 26, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Mabingwa watetezi Azam FC wamejiiamrisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodcaom Tanzania Bara (VPL) licha ya kubanwa kwa sare yan 1-1 na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana jioni.

Sare hiyo imewafanya wanalambalamba Azam FC wafiishe pointi 21 katika mechi 11 wakifuatwa na Yanga SC wenye pointi 18 sawa na JKT Ruvu ambao jana wametoka sare ya 1-1 na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.

Simba SC kama kawaida yao walianza kwa kasi mechi hiyo wakicheza soka lao jipya la pasi fupi fupi za mfumo wa Barcelona aliokuja nao kocha mkuu mpya, Mserbia Goran Kopunovic lakini ilikuwa mbaya kwa kipindi cha pili.

Ilikuwa dakika ya 19 kiungo mshambuliaji wa Simba SC kutoka Mganda, Emmanuel Okwi alipotumia mwanya wa kujisahau kwa beki wa pembeni kulia Shomari Kapombe aliyeingia ndani na kuiacha wingi yake ikiwa haina mlinzi na kumpa mwanya mchezaji huyo zamani wa SC Villa ya Uganda, Etoile du Sahel ya Tunisia na Yanga SC shuti la mguu wa kulia akiwa huru akiitendea haki krosi ya beki mpya wa pembeni kulia Hassan Kessy.

Bao hilo lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza, lilikuwa la nne kwa Okwi msimu huu baada ya kufunga mabao matatu katika mechi nyingine tisa zilizopita akiwa ni kinara wa mabao Simba SC.

Azam FC ndiyo waliofanya mashambulizi mengi zaidi katika mechi hiyo hasa kipindi cha pili lakini safu yao ya ushambulizi ya leo haikuwa vizuri licha ya kuongozwa na kinara wa mabao Mrundi Didier Kavumbagu na kiungo Frank Domayo ambaye amekuwa akichezeshwa katika nafasi ya ushambuliaji tangu apone majeraha yake, akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Mafunzo FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Didier Kavumbagu na mtokeabenchini John Bocco 'Adebayor' walionekana kukosa mbinu za kumfunga kipa kinda Manyika Peter Jr licha ya kupewa pasi nyingi za ndani ya boksi.

Ilikuwa dakika tatu kabla ya saa ya mchezo, mchezajin bora wa VPL msimu uliopita, Kipre Tchetche alipoisawazishia Azam FC akiutendea haki pasi murua ya mtokeabenchini Khamis Mcha iliyopenyezwa ndani ya boksi kutoka Kaskazini Magharibi mwa Uwanja wa Taifa.

Tchetche, pacha wa Michael Bolou wa Azam FC pia, alipiga shuti hilo bila papara kwani alikuwa huru baada ya beki wa pembeni kulia Mohamed Husein 'Shabalala' kuiga makosan ya Kapombe kwa kuingia ndani na kusahau majukumu yake ya kiulinzi.

Hilo ni goli la pili katika mechi mbili mfululizo kwa raia huyo wa Ivory Coast baada ya kufunga pia katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata dhidi ya Kagera Sugar FC Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza Jumanne.
Mfungaji huyo bora wa VPL msimu wa 2012/13, Tchetche amecheza mechi tisa kati ya 11 ambazo kikosi cha Azam FC kimecheza kwa sasa. Alikosa mechi mbili walizolala 1-0 dhidi ya JKT Ruvu na Ndanda FC baada ya kurejea kwao kutatua kile kilichoelezwa na uongozi wa Azam FC kuwa ni matatizo ya kifamilia.

OKWI APOTEZA FAHAMU
Katika saa ya mchezo, Simba SC ilipata pigo Simba SC ilipata pigo baada ya Okwi kupoteza fahamu na kulazimika kuondolewa uwanjani kwa machela kisha kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia kugongana na beki Aggrey Morris wa Azam FC nje kidogo mwa boksi la vinara hao wa msimamo wa ligi.


Daktari aliyempima Okwi kwenye Uwanja wa Taifa na kumpatia huduma ya kwanza, Richard Yomba, amesema mchezaji huyo amepelekwa Muhimbili akiwa amezinduka na kusema anajisikia maamivu makali ya shingo.

MBEYA DERBY HAKUNA MBABE
Katika mechi ya watani wa jadi jijini Mbeya, Mbeya City FC imelazimishwa sare ya 2-2 usiku baada ya wapinzani wao Tanzania Prisons FC kusawazisha dakika ya 89.

Prisons inayonolewa na David Mwamaja, kocha wa zamani wa Simba SC, ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa beki Boniface Hau katika dakika ya saba tu ya mchezo lakini kikosi cha kocha bora wa VPL msimu uliopita, Juma Mwambusi kilicharuka na kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Oljoro JKT, Paul Nonga kabla ya winga wa zamani wa Kagera Sugar FC, Themi Felix kuandika la pili kwa shuti kali la nyuzi 90 katika dakika ya 49.  

Dakika moja kabla ya kumalizika kwa mechi hiyo, beki kisiki anayetajwa kuwa kiboko ya Amisi Tambwe, Nurdin Chona aliifungia Tanzania Prisons bao la kusawazisha la 'usiku' na kuwanyamazisha mashabiki wa City ambao waliamini timu yao ingeibuka na ushindi. 

KAGERA SUGAR FC 1-2 NDANDA FC
Kagera Sugar FC wamepata kipigo cha tatu mfululizo katika uwanja ao mpya wa CCM Kirumba, Mwanza baada ya kukubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Ndanda FC.

Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Juma Mpola kipindi cha kwanza lakini Ndanda Kuchele wakafanya kweli kwa kusawazsha kupitia kwa Stamini Mbonde kabla ya kupata la ushindi kupitia kwa Nassoro Kapama.

Kagera Sugar FC ambayo ni timu pekee msimu huu iliyozifunga Simba SC na Yanga SC, haijashinda mechi hata moja tangu ihamie Mwanza kupisha ukarabati wa Uwanja wa Kaitaba, ikifungwa 1-0 na Mbeya City FC, 3-1 na Azam FC na kipigo cha  leodhidi ya Ndanda FC.


RUVU YAVUNJA MWIKO MTIBWA 
Baaada ya kuibana Yanga SC Jumamosi ya Januari 18 na kusababisha kufungiwa kwa refa Mohamed Teofile wa Morogoro, Ruvu Shooting Stars imevunja mwiko baada ya kuichapa Mtibwa Sugar FC 2-1 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Mtibwa Sugar FC wanaonolewa na nahodha wao wa zamani na Taifa Stars, Mecky Mexime, walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Jamal Mnyate lakini walikuwa ni Hamis Maulid na Seleman waliokipa ushindi kikosi cha Mkenya Tom Alex Olaba na kuvunja mwiko wa Mtibwa Sugar FC kutofungwa msimu huu.

Kabla ya kipigo cha leo, Mtibwab Sugar FC ilikuwa imecheza mechi nne mfululizo ikiambulia sare za 1-1 katika mechi hizo zote dhidi ya Simba SC, Kagera Sugar FC, Stand United na JKT Ruvu.

STAND WAONDOKA KWA ULIZNI WA POLISI
Kama kawaida yake, Stand United FC imeendelea kufanya vibaya kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kambarage usukumani mjini Shinyanga baada ya kupata kipigo1-0 dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union leo jioni.

Bao pekee la mechi hiyo limefungwa na Godfrey Wambura dakika ya 42 na kuwafanya mashabiki wa Stand United FC kuwavaa viongozi wa timu hiyo wakitaka kuwapiga kwa matokeo mabovu nyumbani.

Ligi hiyo itaendelea Jumatano kwa mechi moja kwenye Uwanja wa Taifa kati ya Simba SC na Mbeya City FC, mechi hiyo ni ya kiporo cha raundi ya 10.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video