
Andrey Coutinho (kushoto) na Kpah Sherman (kulia) wataonesha makali leo?
LIGI kuu soka Tanzania bara raundi ya 12 inaendelea
leo kwa mechi moja kupigwa uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro kati ya wenyeji
Polisi Morogoro na Yanga.
Hii ni mechi ya tatu ya ligi kuu kwa kocha wa
Yanga, Hans van der Pluijm tangu arejee kuifundisha klabu hii akirithi mikoba
ya Marcio Maximo.
Katika mechi mbili za kwanza, Pluijm hajapata
ushindi kwani alitoka sare ya 2-2 na Azam fc na mchezo uliopita alivuna pointi
moja pia kufuatia suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shootings. Mechi
zote zilipigwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Kikosi cha Yanga kinachoaminika kuwa na
washambuliaji wakali akiwemo Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Saimon Msuva, Danny
Mrwanda na Andrey Coutinho katika mechi tatu zilizopita kilikuwa butu katika
umaliziaji wa pasi za mwisho na ikawalizimu baadhi ya wanachama kufikiria
kuomba dua ya kutoa nuksi.
Ligi kuu iteandelea tena kesho jumapili kati ya Azam na Simba (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar na Ndanda
(Uwanja wa CCM Kirumba), Stand United na Coastal Union (Uwanja wa Kambarage),,
Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Ruvu Shooting na Mtibwa
Sugar (uwanja wa Mabatini), na JKT Ruvu na Mgambo Shooting (Uwanja wa Azam
Complex).
0 comments:
Post a Comment