Thursday, January 8, 2015


K 01
Na Bertha Lumala
TIMU ya Kikapu ya Polisi imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Karume inayoendelea visiwani hapa baada ya kuitungua New West vikapu 62-42 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Maisara jana.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali lakini walikuwa ni Polisi waliokwenda mapumziko wakiwa mbele kwa vikapu 22-10.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu na Polisi kuendelea kuongoza katika robo ya tatu ambayo iliimaliza ikiwa na vikapu 45-25 katika kipindi hicho.

Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ni African Magic, Rangers na Stone Town. Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kuchezwa leo jioni kati ya African Magic na Stone Town.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video