Monday, January 12, 2015

Na Bertha Lumala
Timu ya kikapu ya Polisi imetwaa ubingwa wa michuano ya Mapinduzi kwa kuifunga Stone Towne vikapu 89-58.

Mchezo huo wa fainali ulichezwa jana Uwanja wa Maisara visiwani hapa ukianza kwa ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote.

Hata hivyo, walikuwa ni Polisi waliodhihirisha kuwa wababe wa Stone Towne kwa kuongoza katika robo zote na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo mnono.

Mgeni rasmi wa pambano hilo alikuwa Mwakilishi wa Wizara ya Habari na Teknolojia ya Kenya, Dickson Nyandiga,  ambaye alimkabidhi bingwa Sh. 250,000 na mshindi wa pili Sh.150,000.

Timu sita zilishiriki michuano hiyo ambazo ni mabingwa Polisi, Stone Towne, JKU, Rangers, African Magic na New West. Mashindano hayo yalisimamiwa na Chama Cha Kikapu Zanzibar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video