Andrea Pirlo
Kiungo mchezeshaji wa klabu juventus turin Andrea Pirlo
ameibuka na kusema kuwa mchezaji Paul Pogba ataingia katika historia endapo
kama atabaki katika kiwango alichonacho hivi sasa.
Paul Pogba
Pogba raia wa ufaransa mwenye umri wa miaka ishirini na moja
alitua katika dimba la turin kwa uhamisho wa bure katika majira ya joto mwaka
2012 akitokea katika klabu ya Manchester united na tangu hapo amekuwa kiungo
mwenye uwezo mkubwa ambaye kwa sasa anamezewa mate na klabu kubwa.
mchezaji huyo anahusishwa na kujiunga na klabu mbalimbali
ikiwepo klabu yake ya zamani Manchester united, mabingwa wa ulaya Real Madrid,
Chelsea pamoja na mabingwa wa ligi kuu nchini ufaransa klabu ya paris saint
germain licha ya wakala wake kutamka kwamba atasalia klabuni hapo mpaka mwisho
wa msimu huu.
Pirlo ambaye amekuwa akishirikiana na pogba katika nafasi ya kiungo kwa miaka
miwili na nusu sasa ametabiri makubwa kwa kinda huyo ambaye yupo katika kiwango
cha juu kwa sasa.
"Pogba hajaacha kuimarika siku hadi siku,ana kila kitu kuwa mchezaji bora
duniani embapo kama ataweka kichwa chake mabegani na kuongeza bidii ataweka
historia kubwa katika mchezo wa soka,”mkongwe Pirlo aliliambia gazeti la
Telefoot.
0 comments:
Post a Comment