Monday, January 5, 2015


Ili kuinua kiwango cha soka visiwani Zanzibar, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm ameshauri timu za visiwa hivyo zishiriki pia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Pluijm aliyerejea nchini kuinoa Yanga baada ya kutimuliwa kwa Mbrazil Marcio Maximo, aliyasema hayo katika mahojiano na waandishi wa habari mara tu baada ya kumalizika kwa mechi yao ya pili ya Kundi A la michuano ya Kombe la Mapinduzi waliyoshinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Polisi FC Uwanja wa Amaan visiwani hapa jana jioni.
Kocha huyo alishauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) wakae meza moja kuangalia uwezekano kuwa na ligi inayoshirikisha timu zote za Ligi Kuu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
“Tumeshinda kwa idadi kubwa ya mabao mechi zetu mbili za mwanzo za kundi letu (Kundi A) kwa sababu hatujapangwa na wapinzani wa kweli. Soka la Zanzibar liko chini, ninafikiri kuna haja timu za Zanzibar kushiriki VPL.
“Timu za Zanzibar zina wachezaji wazuri na wenye vipaji lakini hazina zinakosa ushindani. Ninafikiri zikishiriki VPL zitakuwa timu bora ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati,” ,” alisema Pluijm.
Alisema anatambua suala hilo litakuwa gumu kutokana na hali ya siasa iliyopo nchini huku akisisitiza kuwa jitihada zinapaswa kufanyika kuongeza ubora wa soka visiwani hapa.
Yanga SC imepangwa kundi moja na Polisi Zanzibar, wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika inayoanza mwezi ujao, Shaba FC ya Pemba inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar na Taifa ya Jang’ombe inayoshiriki Ligi Daraja la Pili visiswani hapa.
Miongo kadhaa iliyopita, timu za Tanzania Bara na Zanzibar zilikuwa zikichuana katika mashindano ya Kombe la Muungano.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video