Manuel Pellegrini akitazama mbinguni baada ya kuchapwa 2-0 na Arsenal
Olivier Giroud (kulia) akipiga kichwa na kumfunga kipa wa Man City Joe Hart .
Manuel Pellegrini amekiri kuwa kama Manchester City wanataka kuteteta ubingwa wa ligi kuu England, EPL, lazima waifunge Chelsea.
Pellegrini amesema hayo kufuatia kuambulia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika mechi ya ligi kuu iliyopigwa jana uwanja wa Etihad.
City walifungwa na Santi Cazorla kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 24, na baadaye mshambuliaji aliye kwenye ubora Olvier Giroud aliandika bao la pili kwa njia ya kichwa dakika ya 67.
Kipigo hicho kimewafanya Man City wawe pointi tano nyuma ya Chelsea ambao waliifunga Swansea mabao 5-0 jumamosi iliyopita.
Man City watasafiri januari 31 mwaka huu kwenda Stamford Bridge ambapo watachuana na wenyeji Chelsea.
"Lazima tupunguze pengo mpaka kufikia mbili. Natumaini tutarudi katika kiwango chetu cha kawaida.
" Mchezo wa Chelsea utakuwa mgumu sana. Tutajitahidi kushinda mechi hiyo kupunguza pengo la pointi".
0 comments:
Post a Comment