
MICHUANO ya Mataifa ya Africa, Afcon, inaanza
kutimua vumbi leo (januari 17) kuanzia
majira ya saa 1:00 usiku nchini Guinea ya Ikweta kwa mechi mbili za kundi A kupigwa.
Mechi ya ufunguzi itawakutanisha Guinea ya Ikweta
dhidi ya Congo katika kipute cha cha kwanza cha kundi A uwanja wa Estadio de
Bata.
Mechi ya pili ya kundi hilo itakuwakutanisha Burkina
Faso na wenyeji Gabon katika uwanja huo huo.
Kesho januari 18, Zambia wataoneshana kazi na Congo
DR katika mechi ya kundi B itakayopigwa
uwanja wa Nuevo Estadio de Ebebiyín, baadaye Tunisa watachuana
na Visiwa vya Cape Verde.
Jumatatu januari 19, timu ya taifa ya Ghana, Black Stars
itashuka dimbani kuchuana na Simba Wateranga, Senegal katika mechi ya kwanza ya
kundi C itayopigwa uwanja wa Estadio de Mongomo.
Mechi ya pili ya kundi C itawakutanisha Aligeria dhidi ya
Africa kusini katika uwanja huo huo.
Tutaendelea kuwajuza ratiba ya michuano hii.
0 comments:
Post a Comment