MIAMBA ya soka kutoka Magharibi mwa Afrika, Ivory
Coast 'Tembo' imeanza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Guinea katika mechi ya kundi D ,
michuano ya mataifa ya Afrika inayoendelea huko Guinea ya Ikweta.
Guinea walikuwa wa kwanza kufunga goli katika
dakika 36’ kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wake Mohamed Yattara, hata
hivyo Ivory Coasta walisawazisha dakika ya 72’ kupitia kwa Seydou Doumbia.
Nayo mechi ya pili ya kundi kund hilo baina ya
Mali na Cameroon imemalizika kwa sare ya 1-1.
Mali waliandika bao la kuongoza dakika ya 71’
kupitia kwa Yambou Yatabare, lakini Simba wasiofugika, Cameroon wakasawazisha
kupitia kwa Ambroise Oyongo Bitolo.
Kufuatia kumalizika kwa mechi za kwanza za kundi
D, michuano hiyo leo inaendelea kwa mzunguko wa pili wa makundi.
Timu za kundi A zinaanza kutupa karata yao ya pili
ambapo mechi ya kwanza itawakutanisha wenyeji Guinea ya Ikweta dhidi ya
Burkinafaso ambao walipoteza mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 dhidi ya Gabon.
Mechi ya pili inayoanza majira ya saa 4:00 usiku
leo, itawakutanisha Congo na Gabon.
0 comments:
Post a Comment