KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic
amemuweka benchi kipa mkongwe Ivo Mpaunda licha ya kuipa ubingwa wa kombe la
Mapinduzi januari 13 usiku mwaka huu akidaka penalti ya mwisho vya Vicent
Baranabas, Mmyama akishinda kwa matuta 4-3.
Goran amemuanzisha kipa kijana, Manyika Peter,
huku akisaidia na beki wa kulia Hassan Ramadhan
Kessy na beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Mabeki wa kati ni Hassan Isihaka na Juuko
Mursheed. Kiungo wa ulinzi ameanza Jonas Mkude.
Winga wa kulia ameanza Ramadhani Singano, wakati
kiungo namba nane ni Said Hamis Ndemla.
Mshambuliaji wa mwisho ni Danny Sserunkuma, wakati
nyuma yake ameanza Elius Maguri na winga wa kushoto ni Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa akiba ni Ivo Mapunda, Masoud Nassor ‘Cholo’,
Abdi Banda, Awadh Juma, Ibrahim Hajib, Shaaban Kisiga na Simon Sserunkuma.
Kikosi cha Ndanda ni: Salehe Malande, Azizi Sibo,
Paul Ngalema, Kassian Ponera, Ernest Mwalupani, Zabron Raymond, Stamili Mbonde,
Omega Seme, Omary Mponda, Gideon Benson, Jacob Masawe.
Wachezaji wa akiba: Wilbert Mweta, Shukuru
Chachala, Hemed Khoja, Nassoro Kapama, Masoud Ally, Said Issa, Salum Minelly.
0 comments:
Post a Comment