KIUNGO mshambuliaji wa Simba Sc, Mganda Emmanuel
Anord Okwi anatarajia kuivaa JKT Ruvu kesho uwanja wa Taifa katika mechi ya
ligi kuu Tanzania bara.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amezungumza
na mtandao huu dakika chache zilizopita akiwa uwanja wa mazoezi wa JKT Mbweni
ambapo Simba inaendelea na mazoezi hivi tunavyoongea na kueleza kuwa Okwi yuko
fiti na atacheza mechi ya kesho.
“Nipo hapa uwanjani JKT Mbweni, Okwi anaendelea na
mazoezi. Kesho atacheza”. Amesema Nyasio.
Pia Nyasio amesema beki wa pembeni Hassan Ramadhan
Kessy yuko fiti kucheza kesho na muda huu unaendelea na mazoezi.
Hata hivyo, Afisa habari huyo amesema Simba
itaendelea kuikosa huduma ya kiungo Said Hamis Ndemla ambaye bado anasumbuliwa
na majeruhi.
Okwi, Ndemla na Kessy waliikosa mechi ya jumatano
iliyopita uwanja wa Taifa ambapo Mnyama Simba alichapwa 2-1 na Mbeya City.
Nyasio amesema kesho watapambana kupata ushindi,
licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto katika michuano ya ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment