Thursday, January 29, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC kutoka Uganda, Emmanuel Okwi amejikuta akilia kama mtoto mdogo baada ya timu hiyo ya Msimbazi jijini kugongwa nyundo mbili na Wagonga Nyundo wa Mbeya, Mbeya City FC katika mechi pekee ya jana ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa jijini hapa.

Kikosi cha Kocha Bora wa msimu uliopita wa VPL, Juma Mwambusi cha Mbeya City FC kilitoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 katika mechi hiyo ya kiporo ya raundi ya 10 iliyopaswa kuchezwa Uwanja wa Taifa Januari 11 mwaka huu lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 visiwani Zanzibar Januari 1-13.

GOLI LA SIMBA SC 
Wakionekana wazi kuhitaji huduma ya Okwi anayejiuguza baada ya kupoteza fahamu uwanjani katika mechi yao iliyopita waliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC Jumapili, Simba SC walitangulia kufunga kupitia kwa mshambuliaji Ibrahim Hajib, mfungaji bora wa wekundu hao wa Msimbazi katika michuno ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, aliyeiandikia timu hiyo bao katika dakika ya 22 akifumua shuti kali la takriban mita 23 la 'fri-kiki' lililokwenda moja kwa moja langoni mwa wageni na kuwalipua kwa shangwe mashabiki wachache wa Simba SC waliojitokea uwanjani.

Hilo ni bao lake la kwanza msimu huu wa VPL na la nne kwake msimu huu baada ya kuifungia Simba SC mabao matatu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwezi huu sawa na Andrey Coutinho wa Yanga SC, Willian Wadri wa KCCA ya Uganda na Amour Omary Janja wa JKU FC ya Zanzibar.
Bao hilo lilidumu katika kipindi chote cha kwanza huku Mbeya City FC ikionekekana kucheza chini ya kiwango ikijilinda kwa muda mwingi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni kwa wenyeji huku winga wake mkongwe Themi Felix iliyemnasa baada ya kumalizika kwa msimu uliopita kutoka Kagera Sugar FC akionekana kukosa mbinu za kuwatoka mabeki wa pembeni wa Simba SC.

CITY WASAWAZISHA
Beki wa pembeni kushoto wa Mbeya City FC anayesifika kwa kurusha mipira kama kona, Hamad Kibopile aliisawazishia City akifumua shuti la mguu wa kushoto ambalo kipa kinda, Manyika Peter Jr alibaki amesimama bila kujishughulisha kwa lolote. Mpira ulipigwa kama krosi lakini ukaingia nyuzi 90 ya lango la Kusini la Uwanja wa Taifa ambalo City walilitumia pia kusawazisha mabao mawili ya Simba SC msimu uliopita katika sare yao ya 2-2 mwaka juzi.

PENALTI YA CITY
Katika dakika ya kwanza ya dakika tatu za nyongeza, City walifanya shambulizi la kushtukiza Rafael Dauda alipowatoka mabeki wa Simba SC kisha kukwatuliwa na kipa Manyika Jr ndani ya boksi na kuzaa penalti iliyofungwa na Yusuph Abdallah.

MANYIKA Jr ALISTAHILI NYEKUNDU
Katika hali ya kushangaza na iliyozoeleka kuiona kwa marefa wa Tanzania, refa Kambuzi alimwonesha kadi ya njano badala ya kumtoa kwa kadi nyekundu kipa Manyika Jr kwa mujibu wa Sheria Na. 12 ya Soka (Makosa na Tabia Mbaya) kwa kuwanyima wapinzani bao kwa kumkwatua mchezaji wa timu mpinzani ikiwa ni moja ya makosa saba yanayomtoa mchezaji moja kwa moja uwanjani kwa kuoneshwa kadi nyekundu.

Kambuzi alionekana kutaka kumtoa kwa kadi nyekundu kipa huyo lakini akasita baada ya wachezaji wengi wa Simba SC kumvaa na kumzonga kabla ya tuta hilo kupigwa. 

CHOLLO AKOSA PENALTI
Sekunde chache kabla ya mechi kumalizika, Simba SC nao wakapewa 'tuta' lililojaa utata, refa Kambuzi kutoka usukumani mkoani Shinyanga akidai beki Hassan Isihaka alichezewa rafu na wachezaji wa City ndani ya boksi, tuta ambalo hata hivyo beki wa pembeni kulia na nahodha wa zamani wa Simba SC, Nassoro Masoud 'Chollo' aligongesha besela na kuinyima timu yake bao la kusawazisha.

Hiyo ni penalti ya kwanza Simba SC wamepewa msimu huu wa VPL iliyoshuhudiwa Chollo akiifanya Simba SC ilale kwa mara ya pili msimu huu, ikiwa na sare 7 na ushindi mara mbili dhidi ya Ruvu Shooting Stars ya Mlandizi, Pwani na Ndanda FC ya Masasi, Mtwara.

OKWI ALIA KAMA MTOTO
Baada ya mechi hiyo kumalizika, kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Okwi ambaye alikuwa jukwaani wakati wa mechi hiyo, alionekana akiingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Simba SC akilia kama mtoto sawa na Chollo, kipa Manyika Jr na wachezaji wengine wengi wa Simba SC.

Kwa kifupi, chumba cha kubadilishia nguo cha Simba SC kilikuwa kimetawaliwa na vilio vya wachezaji huku kukidaiwa kuwa kipa kinda Manyika ameomba asichezeshwe kwenye mechi za LAWAMA kama hiyo.

MASHABIKI SIMBA SC WAPIGWA MABOMU
Mashabiki wasiokuwa na uvumilivu na wenye hasira wa Simba SC walianza kufanya vurugu katika kuonesha kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao. 

Kundi la mashabiki hao lilikusanyika nje ya lango kuu la kuingia Uwanja wa Taifa likijiandaa kulishambulia kwa mawe basi kubwa la Simba SC lililokuwa limebeba wachezaji lakini Jeshi la Polisi lilishtukia mchezo huo mchafu na kuwatawanya mashabiki hao klwa kupiga mabomu ya machozi.


Kilikuwa ni kipigo cha pili kwa Simba msimu huu na cha kwanza kwa kocha Mserbia Goran Kopunovic, ambaye baada ya mchezo alitamka wazi Simba SC isitaraji ubingwa wa VPL msimu huu.

Kipigo kiliwaacha Wekundu wa Msimbazi waendelee kuchechemea kwenye nafasi ya 10 ya msimamo wa VPL, ligi yenye timu 14, Mbeya City FC waliotua jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki kwa ndege, wakipaa kutoka nafasi ya tatu kutoka mkiani hadi nafasi ya saba wakiwa na pointi 15 baada ya mechi 11.

KUIVAA JKT RUVU JUMAMOSI
Simba SC watashuka tena Uwanja wa Tafa mwishoni mwa wiki kumenyana na timu ngumu ya JKT Ruvu Stars ya Pwani iliyoko nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 18 sawa na Yanga SC iliyoko nafasi ya pili kwa faida ya tofauti nzuri ya mabao ya kufunga na kufungwa. 

JKT Ruvu Stars iliifunga Simba SC mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho msimu uliopita Uwanja wa Taifa na msimu huu timu hiyo ya kocha wa zamani wa Yanga SC, mzawa Fred Felix Minziro ni moto wa kuotea mbali kwani ndiyo timu ya kwanza kuwafunga mabingwa waetezi Azam FC waliotwaa ubingwa wa VPL msimu uliopita bila kupoteza hata mechi moja.

Azam FC ilifungwa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam FC jijini hapa Oktoba 25 mwaka jana ikiwa ni kipigo cha kwanza kwa wanalambalamba baada ya kucheza mechi 38 za Ligi Kuu bila kupoteza hata moja.

Bao la kikosi cha Minziro lilifungwa na mshambuliaji hata kwa sasa VPL, Samwel Kamuntu ambaye amefunga mabao manne katika mechi nne mfululizo zilizopita.


Vikosi katika mechi ya jana Taifa vilikuwa; 
Simba SC: Manyika Peter Jr, Nassoro Masoud 'Chollo', Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/ Twaha Ibrahim (dk 62), Awadh Juma, Ibrahim Hajib, Dan Sserunkuma/ Elias Maguli (dk 46) na Ramadhani Singano 'Messi'.

Mbeya City FC: David Burhan, Richard Peter, Hamad Kibopile, Juma Nyoso, Steven Mazanda, Yusuph Abdallah, Themi Felix 'Mnyama'/ Hamidu Mohamed (dk 69), Raphael Alfa, Paul Nonga, Cosmas Lewis/ Peter Mapunda (dk 66) na Deus Kaseke/ Idrisa Rashid (dk 78).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video