KIKOSI cha Mbeya City fc kipo safi asilimia 100
kuwavaa Polisi Morogoro ikisaka mzigo mwingine wa pointi tatu katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara itayopigwa jioni
ya leo uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Taarifa iliyopenyezwa MPENJA BLOG asubuhi hii na
Afisa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten inasema hakuna majeruhi yoyote na jana
jioni walifanya mazoezi vizuri na wanaamini wako tayari kuchukua pointi tatu
kama Mungu atawaajalia.
“Timu iko vizuri, hakuna majeruhi. Kama unavyoona
sahizi ukishinda mechi moja unapanda sana kwenye msimamo. Tukishinda leo
tutapanda zaidi. Tumejiandaa kikamilifu”. Amesema Dismas.
Mbeya City fc inaingia uwanjani ikiwa na
kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 iliopata jumatano iliyopita uwanja wa Taifa
dhidi ya Simba sc.
0 comments:
Post a Comment