KUTOKANA na mwenendo mbovu wa Simba SC katika
mechi za ligi kuu Tanzania bara, mchezaji wa zamani wa timu hiyo na kiongozi wa
TFF, Mtemi Ramadhani amefanya mahojiano maalumu na mtandao huu na kuweka wazi
sababu za Mnyama kuzidi kuboronga.
Mwandishi:
Mtemi Ramadhani, wewe ni mchezaji wa zamani wa Simba, sasa hivi kumekuwa na
malalamiko mengi ya wanachama na wapenzi wa Simba kuhusu mwenendo wa timu yao,
kwa uzoefu wako wa kuwa kwenye mpira kwa miaka mingi unafikiri nini kinawasibu
Simba saha hivi?
Mtemi: Suala la Simba liko wazi, mwenye kujua
mpira anajua kwasababu mpira hauchezwi vyumbani, mpira unachezwa hadharani.
Timu ilivyocheza Zanzibar kila mtu aliona, timu inavyocheza hapa kila mtu
anaona, tatizo la Simba ni kwamba vijana wa Simba hawataki mazoezi.
Timu ya Simba haina mazoezi magumu, suala lao ni kwamba
hawataki mazoezi. Simba wamecheza mechi sita kule Zanzibar, zilikuwa za
mfululizo na walikuwa kambini, lakini baada ya pale walirudi kucheza na Ndanda.
Nasikia tena wakafanya kambi siku moja kabla ya mpira, huwezi kucheza mpira
bila kufanya mazoezi magumu hata siku moja, haiwezekani.
Simba hawajajiandaa vya kutosha, Simba ikicheza na
timu yoyote inayofanya mazoezi magumu, ya kukimbia huku na kule, haiwezi
kushinda kwa pumzi ile.
Na jambo zuri zaidi ni kwamba mipira inaonekana
kwenye ligi nzuri, kama ni Afcon, kama ni Barcelona, Real Madrid, wanaona duniani kote ambavyo mpira umebadilika,
watu wanacheza kwa nguvu, wanakimbia, wanakaba. Simba mpaka mchezaji apate
mpira ndio beki anakwenda kukaba, kwahiyo anatoa pasi kwa mwingine ambaye
hajakabwa.
Simba hawezi kucheza mpira wa namna hiyo, hata
iweje, na wanaweza kushuka daraja hivi hivi, si jambo la kuamini, lakini si la
ajabu.
Mwandishi:
Lawama kubwa zinatupiwa kwa uongozi, unafikri utawala nao unachangia mwenendo
mbaya wa timu?
Mtemi: Naweza nikasema ndiyo! Ingawa si kwa asilimia
kubwa. Lakini wanapaswa kusimamia timu, hawa walimu wa kizungu wana tatizo
moja, tulikuwa na mzee mmoja alikuwa anaitwa Jan Poulsen pale TFF, timu
ikifanya mazoezi asubuhi jioni anasema walale, ukimwabia tufanye hiki, anasema
siku mbili wapumzike.
Binafsi niliwahi kuongea na mwalimu yule, akasema
unajua mpira wa siku hizi hautaki mbio sana, si unao Barcelona wanavyocheza.
Sasa ni jukumu la viongozi kusimamia, mwalimu anaweza kutoka na mambo yake ya
ulaya, kamati ya utendaji inatakiwa imuite na kumwambia, “Bwana wachezaji wa
Kiswahili wako moja, mbili, tatu na bila kufanya moja, mbili, tatu,hatuwezi
kwenda”.
Sasa unamwachia mwalimu wa Kizungu ambaye anakuja
na falsafa ya watu wa nje ambako wachezaji wanajitambua, wanalala majumbani
kwao, wana mapesa mengi, mtu anatambua wajibu wake.
Hawa wa kwetu sio siri hawajitambui, tunawaona,
mtu anatoka mazoezini na gari yake ndani
ana mwanamke, mwingine utasikia nusura apigwe chupa Kinondoni kwasababu ya
kugombania mwanamke, hao ni wachezaji wa Simba, huwezi kucheza mpira namna
hiyo.
0 comments:
Post a Comment