Thursday, January 29, 2015



Kikosi cha Mtibwa Sugar
Baada ya kupoteza mchezo wake uliopita wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya wapiga kwata klabu ya maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa mabatini mkoani pwani,klabu ya Mtibwa Sukari kutoka Manungu Turiani mkoani Morogoro imetamba kuigalagaza klabu ya wagosi wa kaya wagosi wa ndima Coastal Union wikiendi hii mchezo utakaochezwa katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Akizungumza na Mpenja Blog afisa habari wa klabu hiyo Thobias Kifaru amesema kweli wamepania kuiangamiza Coastal Union baada ya kupoteza dhidi ya Ruvu Shooting endapo kama mwamuzi atafuata sheria zote kumi na saba za soka.

“Baada ya kupoteza mchezo wetu dhidi ya ndugu zetu kikosi cha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa nguvu zetu tumezielekeza katika mchezo unaofuata ambapo tunaifuata Coastal Union jijini Tanga wikiendi hii na kuhakikisha kuwa tunapoza machungu ya kufungwa na Ruvu Shooting kwa kuinyuka Coastal Union,”alisema kifaru.

Kifaru alisema kuwa anaamini wana kikosi kizuri ambacho kina uwezo wa kutwaa kombe la ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu, licha ya kuporomoshwa katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi ambayo wamekuwa wakiishikilia kwa muda mrefu bila kupoteza mchezo ata mmoja.

“Mtibwa Sukari ina kikosi kizuri chini ya kocha Mecky Mexime,kuna washambuliaji wazuri wakiongozwa na mkongwe Mussa Hassan Mgosi pamoja na Ame Ali Zungu wachezaji ambao ukiwauliza Simba na Yanga wanawafahamu vilivyo kwa kuzisumbua ngome zao za ulinzi katika michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara, kwa hiyo naamini kuwa bado ligi inaendelea na tutafanya vizuri katika michezo inayofuata na atimaye kutwaa kombe la ligi msimu huu,” alijinadi Thobias Kifaru.

Mtibwa Sukari sasa ipo katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara nyuma ya vinara mabingwa watetezi wa ligi kuu klabu ya wanalambalamba Azam fc yenye pointi 21 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 18, Jkt Ruvu pointi 18 na Mtibwa pointi 17.

Na Frank M Mgunga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video