Sunday, January 4, 2015


Baada ya kufunga mabao matatu 'hat-trick katika mechi yao ya kwanza ya Kundi A la Kombe la Mapinduzi waliyoshinda 4-0 dhidi ya Taifa ya Jang'ombe kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzinar, winga Simon Msuva ametoa siri ya mafanikio yake.

Msuva alikuwa mwiba mkali katika mechi hiyo akifunga mabao matatu dakika ya 13,49 na 64 kabla ya kupika bao la nne lililowekwa kambani na mshambuliaji Mliberia Kpah Sherman katika dakika za majeraha.

Akizungumza na mtandao huu visiwani hapa, Msuva amesema: "Juhudi, kujituma mazoezini na wakati wa mechi ndiyo siri ya mafanikio yangu. Pia ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa kunipa ushirikiano mkubwa. Mafanikio yangu ni yao pia."

Mbali na kupewa mpira wa hat-trick, Msuva alikabidhiwa zawadi nyingine baada ya kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo. Mchezaji bora wa kila mechi ya Kombe la Mapinduzi anateuliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (Zaswa) kwa kushirikiana na jopo la makocha.

Msuva sasa ni kinara wa mabao ya michuano hiyo akifuatwa na Amour Omary wa JKU mwenye mabao mawili aliyoyafunga katika mechi zao za Kundi C B dhidi ya Mafunzo FC na Mtibwa Sugar FC.

Winga huyo ambaye anawaniwa vikali na Simba SC -- Msuva, ana mabao manne katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), moja nyuma ya kinara Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC.

Wachezaji wengine wenye mabao manne VPL ni Mkenya Rama Salim wa Coastal Union, Danny Mrwanda wa Yanga SC, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC na Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video