Wednesday, January 7, 2015


13
Na Bertha Lumala
Mpinzani wa Simba SC katika hatua ya robo-fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar amepatikana kwa kurusha shilingi baada ya timu mbili za Kundi A, Polisi na Taifa ya Jang'ombe kumaliza katika nafasi moja.

Polisi, wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu, na Taifa ya Jang'ombe jana walimaliza mechi zao za hatua ya makundi wakitoka suluhu Uwanja wa Mao Tse Tung visiwani hapa.

Matokeo hayo yaliwafanya wote wamalize nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Yanga SC wakiwa wakifanana kwa kila kitu baada ya wote kufungwa na Yanga SC 4-0 kisha wote kuifunga Shaba FC ya Pemba bao 1-0.

Baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu hizo jana, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na Kamati ya Mashindano hayo walikutana na kuamua lifanyike zoezi la kurusha sarafu Uwanja wa Amaan kabla ya kuanza kwa mechi ya mwisho ya Kundi A ya Yanga SC dhidi ya Shaba FC saa 2:15 usiku.

Baada ya sarafu kurushwa kwa sarafu na Kamishina wa mechi ya Yanga SC dhidi ya Shaba FC, Polisi Zanzibar waliibuka kidedea wa bahati nasibu hiyo, hivyo kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa Kundi A wakifanikiwa kuikwepa Simba SC katika mechi ya leo usiku ya robo-fainali ya kwanza Uwanja wa Amaan.

Mechi nyingine tatu za robo-fainali za michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tisa tangu ianzishwe kuenzi Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar yaliyofanywa Januari 12, 1964, zitapigwa kesho Azam FC wakiwavaa Mtibwa Sugar FC, mabingwa watetezi KCCA ya Uganda wakiumana na wawakilishi wa Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwaka huu, Polisi Zanzibar kabla ya Yanga SC kuwakabili maafande wa JKU.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video