Monday, January 5, 2015

KOCHA wa Real Sociedad, David Moyes ameisifu ngome yake ya ulinzi baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Barcelona jana jumapili.

Moyes alikuwa na furaha kidogo mwaka jana, lakini amekuwa na furaha kubwa baada ya timu yake kuichapa Barca kufuatia wao wenyewe kujifunga goli katika dakika ya pili kupitia kwa Jordi Alba.

Mscotish huyo alikuwa na msimu mgumu Manchester United kabla ya kufukuzwa mwezi Aprili mwaka jana na kuamua kukubali kazi ngumu ya kuifundisha Sociedad inayopambana kukwepa kushuka daraja tangu mwezi novemba mwaka jana.

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa katika vyombo vya habari vya Hispania juu ya Moyes kukosa uzoefu wa soka la nchini hiyo, kutojua lugha ya Kihispania, lakini ameanza kwa ugumu, ameimarisha timu kuanzia beki na wamepoteza mechi moja tu mpaka sasa.

“Nina furaha sana kupata matokeo, ilikuwa mechi muhimu na ngumu,” Moyes aliwaambia waandishi wa habari.


“Tulifanya jitihada kubwa ya kulinda na tulijilinda kwa sehemu kubwa ya mechi. Huwezi kushinda mechi kama hujilindi vizuri. Kwa namna tulivyocheza katika safu ya ulinzi kumefanikisha kupata ushindi huu”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video