Monday, January 19, 2015


Demba Ba (left) slots past Simon Mignolet after Gerrard's slip at Anfield at the end of last season
Demba Ba (kushoto) akimfunga Simon Mignolet baada ya Gerrard kuanguka katika uwanja wa Anfield  mwishoni mwa msimu uliopita

Jose Mourinho amewaamuru mashabiki wa Chelsea kuacha kuimba nyimbo za kumbeza Steven Gerrard ambaye alisababisha Liverpool ikose ubingwa msimu uliopita.
Mashabiki wa Chelsea bado hawasahau mwezi aprili mwaka jana ambapo Gerrard alianguka peke yake na kumruhusu mshambuliaji wa zamani wa Mourinho, Demba Ba kufunga goli.
Mourinho ameenda mbali zaidi akisema kipigo cha 2-0 walichopata Liverpool katika uwanja wa Anfield mwaka jana uliwapa ubingwa Manchester City na kuanzia siku hiyo mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakimbeza Gerrard.

Mashabiki huwa wanaimba: ‘Steve Gerrard, Gerrard, he fell on his f****** a***, he gave it to Demba Ba.’ Hatujaona haja ya kutafsiri kwa sababu za kimaadili.
A closer angle shows the mistake, which Jose Mourinho said gifted Manchester City the Premier League title
Picha hii inaonesha kosa alilofanya Gerrard ambalo Jose Mourinho amesema liliwapa ubingwa  Manchester City.

Nyimbo za kumbeza Gerrard zinatarajia kusikika Anfield kesho jumanne wakati Chelsea inakabiliana na Liverpool kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la Ligi 'Capital One'.
Lakini Mourinho aliyelalamika kuwa Stamford Bridge imekuwa kimya sana, amesisitiza kuwa mashabiki waache kuimba nyimbo hizo za kumbeza nyota huyo anayetaka kwenda Marekani.
Amesema: "Ni mchezaji wa historia wa Liverpool, mchezaji wa kihistoria wa ligi kuu. Ni mpinzani ambaye mara zote nampenda na kumheshimu. Kuna wimbo ambao mashabiki wangu wanaimba, siupendi kabisa".
"Mara zote wimbo unafurahisha, lakini kuimba, kuimba na kuimba hasa kwa mchezaji kama yeye, hapana, anastahili heshima, sihitaji dharau"

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video