Jose Mourinho na Diego Costa wakizungumza wakati wa mechi dhidi ya Liverpool
Jose Mourinho amenuna baada ya chama cha soka England, FA kusema kinamtoza faini Diego Costa kwa kuonesha mchezo usiokuwa wa kiungwana.
Mourinho ameichukia FA na anaamini mfungaji wake anayeongoza kufumania nyavu ametolewa kama mbuzi wa kafara kufuatia kumchezea vibaya beki wa Liverpool, Emre Can.
Kocha huyo wa Chelsea ambaye amewahi kutozwa faini na FA alitakiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho ijumaa kuelekea mechi ngumu dhidi ya Manchester City jumamosi, lakini ameufuta.
Diego Costa alionekana kumkanyaga mguu wa kulia Emre Can kwenye mechi ya nusu fainali ya Capital One dhidi ya Liverpool
Costa anaweza kufungiwa mechi tatu baada ya kutozwa faini na FA kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Can.
Klabu ya Chelsea imefuta ratiba ya mkutano na waandishi wa habari na hatawathubutu hata kumtuma kocha msaidizi, Steve Holland kuzungumza na vyombo vya habari.
Imethibitishwa kuwa kikao cha nidhamu cha FA kitakachokaa kesho kitamuadhibu Costa.
Licha ya Costa kukataa kosa lake, mshambuliaji huyo wa Chelsea anatarajia kufungiwa mechi tatu kuanzia ya jumamosi dhidi ya Man City.
0 comments:
Post a Comment