MABINGWA watetezi wa kombe la Mapinduzi, KCC ya
Uganda wamevuliwa rasmi ubingwa wao kufuatia kufungwa penalty 5-4 na Maafande
wa Polisi Zanzibar katika mchezo wa robo fainali ya pili ya kombe hilo
uliomalizika jioni hii uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshindi wa mechi hiyo amelazimika kupatikana kwa
changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya timu zote kutoka suluhu ndani ya
dakika 90.
Katika mikwaju mitano ya kwanza, timu zote
zilifunga mitatu na kukosa miwili.
Penati ya sita, timu zote zilipata ambapo kwa upande wa Polisi aliyefunga mkwaju huo ni Mohammed Salim na kwa upande wa KCC alifunga Kasule Owen.
Ally Khalid wa Polisi alifunga penati ya saba, wakati, Saimon Namwanja wa KCC alikosa penalti ya saba na kuilaza njaa timu yake.
Kwa ujumla penalti 14 zimepigwa katika robo fainali ya kwanza.
Ally Khalid wa Polisi alifunga penati ya saba, wakati, Saimon Namwanja wa KCC alikosa penalti ya saba na kuilaza njaa timu yake.
Kwa ujumla penalti 14 zimepigwa katika robo fainali ya kwanza.
Dhahiri bahati haikuwa upande wa KCC kwani
walitengeneza nafasi nyingi katika vipindi vyote viwili, lakini washambuliaji wake
walishindwa kuzibadili kuwa magoli.
Waliofunga penalti kwa upande wa Polisi ni Daniel Joram, Mohammed Seif, Abadallah
Mwalimu, Mohammed Salim na Ally Khalid, wakati waliokosa ni Suleiman Makungu na
Juma Ally.
Waliofunga penalti kwa upande wa KCC ni Tom
Masiko, Ronnie Kiseka, Saka Mpima, Kasule Owen, wakati wachezaji waliokosa ni
Ivan Ntege, Wadri Willium na Saimon Namwanja.
Wakati huo huo, kamati ya mashindano ilimtangaza
Tom Masiko wa KCC kuwa mchezaji bora wa mechi ya leo na alipewa zawadi ya king’amuzi
cha Azam TV.
Kwa matokeo haya, Polisi Zanzibar itakutana na
Simba katika mechi ya nusu fainali ya kwanza itakayopigwa januari 10 mwaka huu.
Mechi nyingine ya robo fainali inaendelea muda huu
baina ya Azam fc na Mtibwa Sugar, wakati majira ya saa 2:15 usiku Yanga
watachuana na JKU katika robo fainali ya mwisho.
0 comments:
Post a Comment