WEKUNDU wa Msimbazi Simba wako tayari kuivaa Azam
fc katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam jumapili jioni, januari 25.
Afisa habari wa Simba, Humphrey Nyasio amesema
kikosi kipo shwari na kocha anaendelea kukamilisha programu nzima ya mechi
hiyo.
“Sisi tunaendelea vizuri, wachezaji wote wapo
kambini kasoro waliokuwepo Taifa Stars Maboresho. Tunawarajia leo kuungana na
wenzao na watafanya mazoezi ya pamoja”. Amesema Nyasio.
Aidha Nyasio ameweka sawa mkanganyiko uliopo
miongoni mwa wadau wa soka wakidhani mechi itapigwa kesho januari 24 kama
ilivyopangwa.
“Nashangaa watu wanatangaza mechi ipo kesho
(jumamosi), mechi ni jumapili januari 25. Yalifanyika marekebisho ya ratiba
kutokana na mechi ya jana ya Taifa Stars Maboresho dhidi ya Rwanda”. Ameongeza Nyasio.
0 comments:
Post a Comment