WEKUNDU wa Msimbazi Simba wapo njiani kurudi Dar
es salaam baada ya kuitandika Ndanda fc mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu soka
Tanzania bara iliyopigwa jana uwanja wa CCM Nangwanda Sijano mkoani Mtwara.
Mabao ya Simba yalifungwa na Danny Sserunkuma
dakika ya 32 na Elius Maguli dakika ya 52 kipind cha pili.
Meneja wa klabu hiyo, Nico Nyagawa ameuambia
mtandao huu dakika chache ziliopita kuwa wameondoka alfajiri Mkoani Mtwara na
wanajarajia kuingia mapema mchana jijini Dar es salaam.
“Tupo njiani muda huu, tutafika mapema sana.
Tukitua Dar kila mchezaji atashukia mahala pake, watapewa mapumziko . Mwalimu
atasema ni siku ngapi muda si mrefu” Amesema Nyagawa, mshambuliaji wa zamani wa Simba.
0 comments:
Post a Comment