Wednesday, January 14, 2015

Wachezaji wa Simba wakishangilia na kombe lao

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WEKUNDU wa Msimbazi Simba chini ya kocha mpya, Goran Kopunovic wametwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi kufuatia kuifunga Mtibwa Sugar  penalti 4-3 katika mechi ya fainali iliyopigwa usiku wa leo uwanja wa Amaan, Mjini Zanzibar.

Bingwa wa mashindano hayo alilazimika kupatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.

Katika kipindi cha kwanza, Simba walianza kwa kasi wakilisakama lango la Mtibwa Sugar, lakini wakata miwa hao wa Manungu walikuwa imara kuondosha hatari zote langoni kwao.

Almanusura Emmanuel Okwi aandike goli katika dakika ya 18, lakini shuti lake lilidakwa na kipa Said Mohammed. Dakika hiyo hiyo, Ibrahim Hajibu ‘Mido’ aliachia shuti kali ambalo halikulenga lango.

Simba waliendelea kushambulia lango la Mtibwa na katika dakika ya 21 Jonas Mkude alipiga shuti lililopaa juu ya lango akipokea mpira wa kona uliochongwa na Okwi na kuguswa kidogo na Salim Mbonde wa Mtibwa.


Shujaa Ivo Mapunda alibebwa na wachezaji wenzake

Dakika ya 23, Hajibu alishindwa kumalizia mpira uliotemwa na kipa Said Mohammed kufuatia shuti kali liliopigwa na Danny Sserunkuma.

Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 27 baada ya kumvuta Ally Shomari.

Hajibu alipoteza nafasi nzuri katika dakika ya 45 akishindwa kumalizia pasi ya Danny.

Mpaka dakika 45 zinamalizika, hakuna timu iliyoona lango la mwenzako.

Kipindi cha pili Simba waliendelea kucheza vizuri na kwa kasi na katika dakika ya 56, beki wa kushoto wa Mtibwa, David Charles Luhend alioneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Said Hamis Ndemla

Dakika ya 63 beki wa kulia wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy aliachia shuti kali lililogonga mwamba na kuingia tena uwanjani.

Hajib alikwenda kumuona tena kipa Mohammed, lakini alishindwa kutumia vyema pasi ya Ramadhan Singano ‘Messi’ kufuatia kipa huyo wa zamani wa Yanga kuudaka mpira.

Kocha Kopunovic alifanya mabadiliko katika dakika ya 65 akimtoa Hajibu na nafasi yake kuchukuliwa na Elius Mguli.


Kuingia kwa Maguli kuliongeza kasi ya Simba katika safu ya ushambuliaji.

Katika dakika ya 65, Mtibwa walimtoa Musa Nampaka na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Rajab.

Dakika ya 75 Emmanuel Okwi alikwenda benchi nafasi yake ikachukuliwa na Awadh Juma.

Musa Hassan Mgosi alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 78 kufautia kumchezea vibaya Kessy.

Dakika ya 87 Mtibwa walimtoa Ally Shomari na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Kichuya.

Dakika ya 89 Simba walimtoa Ndemla na nafasi yake kuchukuliwa na Shaaban Kisiga.

Katika dakika ya 90 Mtibwa Sugar walimtoa Ame Ally na nafasi yake kuchukuliwa  na Abdallah Juma.

Kuhakikisha wanatwaa ubingwa, Simba walimtoa Peter Manyika katika dakika ya 90 na nafasi yake kuchukuliwa na Ivo Mapunda.

Mapunda ni mzoefu wa kudaka penalti hakuwaangusha katika mapigo hayo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, hakuna timu iliyoona lango la mwenzako.

Baada ya hapo mikwaju ya penalti ilifuata na Simba ndio walikuwa wa kwanza kupiga.

Waliofunga Penalti kwa upande wa Simba ni Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Danny Sserunkuma wakati Shaaban Kisiga alikosa.

Waliofunga kwa upande wa Mtibwa Sugar ni Ally Lundenga, Shaaban Nditi, , Ramadhan Kichuya, wakati Ibrahim Rajab na Vicent Barnabas walikosa penalti hizo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video