Thursday, January 8, 2015

MAISHA ni safari ndefu…katikati pitapita yangu nimemkuta beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, David Charles Luhende akipumzika maeneo fulani hivi.

Mwandishi: Luhende niaje mkali wangu?


Luhende: Barida mzazi, mishe vipi?


Mwandishi: Mbona kama unawaza hivi?


Luhende: Kiaina Babu! Si unajua maisha safari ndefu.


Mwandishi: kwanini unasema hivyo?


Luhende: Ujue mie mpira bwana ni kazi yangu. Kabla ya kuanza kucheza soka miaka ya nyuma kuna kazi nilikuwa nafanya, daah! Acha tu rafiki yangu.


Mwandishi: Kazi gani hiyo?


Luhende: Mimi ni fundi mekanika kaka, nimetengeneza sana magari huko nyuma. Nakumbuka nilikuwa Napata 300, 400 na nikipata sana 500.


Mwandishi: Ulisomea ufundi mekanika?


Luhende: Hapana, ujanja ujanja tu! Tena baba alikuwa anapenda nifanye kazi hii kuliko hata mpira. Sema mama alipenda sana nicheze mpira.

Hata saizi mtu kama ana tatizo na gari lake aje nifanye kazi,lakini lazima anitoe..hahahahahah!


Mwandishi: umetisha sana kijana, sema tutaonana mida tupige stori vizuri!


Luhende: Poa jomba…unafanya vizuri sana!



Mwandishi: Ahsante kijana wa Mecky Mexime.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video