Monday, January 12, 2015


Bao pekee la Fulgence Maganga limeipa Mgambo Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya maafande wenzao wa Ruvu Shooting katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.

Maganga aliyechuana vikali na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC kusaka mchezaji bora wa mwezi Novemba wa ligi hiyo, alifunga bao hilo dakika moja kabla ya mapumziko.

Licha ya kikosi cha Tom Alex Olaba kufanya mabadiliko kadhaa na kujaribu kusawazisha bao hilo, safu ya ulinzi ya Mgambo Shooting Stars ilisimama vizuri na kuwabana vilivyo maafande hao wa Mlandizi, Pwani.

Hadi kipyenga cha mwisho cha refa Kenny Mapunda kutoka Dar es Salaam kupulizwa, ubao wa matokeo ulikuwa unasomeka Mgambo Shooting Stars 1-0 Ruvu Shooting Stars.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video