AFISA habari wa Ruvu Shootings, Masau Mbwire ameendelea kuwa gumzo baada ye leo ku-post ujumbe kwenye ukurasa wa kundi maarufu la Kijiwe cha Soka Tanzania kwenye mtandao wa kijamii wa facebook akimsifu beki kisiki wa Yanga, Mbuyu Junior Twite.
Maneno yenyewe haya hapa:
"Mbuyu Twite ni moja ya wachezaji ninaowakubali.
Nidhamu yake nzuri, mtulivu, mpole, mnyenyekevu mwenye kujitambua!
Mbuyu Twite hashadadii ujinga, hana muda wa kukaa vijiweni kuvizia mademu wanaojilengesha, kukaa baa kubugia viroba au uchochoroni kuvuta Bangi kama tunavyoshuhudia kwa wachezaji wengine.
0 comments:
Post a Comment