WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamekubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Wagonga Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hamad Kibopile
na Yusuph Abdallah aliyefunga kwa njia ya penalti, wakati la Simba limefungwa
na Ibrahim Hajib ‘Mido’.
Hata hivyo dakika ya mwisho ya mchezo, Masoud
Nassor ‘Cholo’ amekosa mkwaju wa penalti baada ya beki Yusuph kumfanyia
madhambi Jonas Mkude katika eneo la hatari.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Simba ndani ya uwanja
wa Taifa, kwani desemba 26 mwaka jana walifungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa zaidi inakujia...................
Taarifa zaidi inakujia...................
0 comments:
Post a Comment