Monday, January 12, 2015

MBEYA City imeifunga Karonga United ya Malawi mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwenye Uwanja wa Mwakangale mkoani Mbeya, lakini kabla ya hapo ilizuka tafrani iliyosababisha mwamuzi mmoja tu kuchezesha mchezo huo.
Mbeya City ilifanikiwa kuifunga Karonga United mabao 2-0 yaliyofungwa na Keny Ally na Steven Mazanda.Chama cha Soka Mkoani Mbeya (Mrefa) kiliwazuia waamuzi kuchezesha mchezo huo kwa kile kilichodaiwa kwamba haukuwa na kibali ambacho kilipaswa kupelekwa TFF kikiitambulisha Karonga kuwa ni timu kutoka Malawi.
Ilidaiwa kwamba Mrefa ilizuia mechi hiyo kwa kuwa Karonga United haikuwasilisha mapema kibali kutoka Chama cha Soka Malawi (Fam), lakini vurugu za mashabiki waliolipa kiingilio cha Sh3000 ziliilazimisha Mrefa kuruhusu mechi hiyo ichezwe ikiwa na mwamuzi mmoja tu bila wasaidizi wake.
Baada ya nguvu ya mashabiki kuwa kubwa, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi alitoa ushauri kwa viongozi wa Chama cha Soka Kyela (KFA) kukipiga picha kibali cha Karonga na kukituma kwa Mrefa na TFF ili mechi ichezeshwe.
KFA awali ilishindwa kutuma kibali hicho kwa Mrefa kutokana na kutokuwepo umeme wilayani hapa. “Unajua lazima ifike mahala mtu aliyetumwa kuzuia mechi hii atumie busara vinginevyo maafa yatatokea, watu wametoa fedha zao unafikiri watatuelewa hapa? Pigeni picha kibali halafu kitumeni Mrefa na TFF,” alisikika Mwambusi akiwaambia viongozi wa KFA.
Kweli, kibali hicho kilifika kwa wahusika na mchezo ukachezwa ukiwa umechelewa.
Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda, alishangazwa na kitendo cha kamisaa, Sadick Jumbe ambaye aliteuliwa na TFF kusimamia mchezo huo lakini alipofika uwanjani hapo akawazuia waamuzi kuchezesha kwa maelekezo ya Katibu wa Mrefa, Seleman Haroub.
“Kyela hakuna umeme, hivyo tulifuata taratibu zote kwa kuwasiliana na Mwenyekiti wa Mrefa, Elias Mwanjala akiwa Dar es Salaam na alitusaidia kuwasiliana na TFF, tukakubaliwa mechi ichezwe sasa tukashangaa hawa waliotuzuia,” alisema Mapunda.
Jumbe alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema; “Mimi siyo msemaji, mtafuteni Haroub.”
Alipotafutwa Haroub alisema: “Niliambiwa na mkubwa wangu kwamba mechi ile haijakamilisha taratibu isichezwe, sasa unafikiri ningefanya nini?”
Source: Mwanaspoti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video