MBEYA CITY FC imetoka sare ya kufungana goli 1-1
na CDA ya Dodoma katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana uwanja wa Jamhuri
mkoani Dodoma.
Mechi hiyo ilitumika na kocha Juma Mwabusi kama
sehemu ya kuangalia makosa katika kikosi chake kabla ya kuivaa Tanzania Prisons
wikiendi hii uwanja wa Sokoine Mbeya.
City na Prisons ni mahasimu wa jiji la Mbeya na
kila wanapokutana cheche zinawaka moto uwanjani.
Timu zote zitaingia katika mchezo huo wa jumamosi zikiwa
na kumbukumbu tofauti.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, City waliifunga
Kagera Sugar bao 1-0 uwanja wa CCM Kirumba, wakati Prisons walitoka 0-0 na
Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
0 comments:
Post a Comment