Friday, January 23, 2015

WAGONGA Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc wamesema hawana homa yoyote kuelekea mechi ya watani wa jiji, ‘Mbeya Derby’  dhidi ya Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ itayopigwa jumapili januari 25 mwaka huu uwanja wa CCM Sokoine Mbeya.

Afisa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten ameuthibitishia mtandao huu kuwa kikosi cha Mbeya City kipo salama, wachezaji wapo katika morali ya hali ya juu kuhakikisha wanavuna ushindi wa tatu mfululizo.

“Sisi hatuna homa yoyote, mara ngingi tunapokutana na Prisons, historia inatubeba, tumejiandaa na tunaamini tutachukua pointi tatu muhimu”. Amesema Dismas  na kuongeza. “Baada ya ushindi dhidi ya Ndanda na Kagera Sugar, Mwalimu Mwambusi amekuwa na kazi ya kuendeleza mafanikio hayo, amekiandaa kikosi vizuri na bila shaka tutafanya vizuri”

Mbeya City kwa sasa wapo nafasi ya 9 wakijikusanyia pointi 11 nyuma ya Ruvu Shootings wenye pointi 12, ingawa wao wamecheza mechi 11 wakati Wanazambarao wameshuka dimbani mara 9.


City imeshinda mechi tatu, imepoteza mechi nne na kutoa sare mechi mbili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video