Matola (kushoto) akiwa na kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic
KOCHA msaidizi wa Simba, Seleman Abdallah Matola ‘Veron’
ameomba kuacha kazi anayofanya kwasasa na kupangiwa kazi nyingine klabuni au
kujiuzulu kabisa.
Rais wa Simba, Evans Aveva amekiri leo kupokea taarifa
hiyo, lakini wamemuambia aandike barua rasmi na kuifikisha kwa uongozi.
Matola amefikia hatua hiyo kutokana na presha
kubwa iliyopo Msimbazi na sasa anafikiria kurudi Simba B.
Kiungo huyo wa zamani wa Simba amekuwa akitupiwa lawama za kuwa chanzo
cha Simba kufanya vibaya na ndio maana anaomba kuacha kazi ya ukocha msaidizi.
0 comments:
Post a Comment