CHELSEA ikiwa ugenini umeishushia mvua ya mabao 5-0 Swansea City katika mechi ya ligi kuu England iliyomalizika usiku huu.
The Blues walifungua karamu ya mabao katika dakika ya kwanza kupitia kwa Mbrazil, Oscar katika dakika ya 1’ ya mchezo.
Mshambulizi hatari wa kimataifa wa Hispania, Diego Coasta aliifungia Chelsea bao la pili katika dakika ya 20’ na bao la tatu katika dakika ya 34’.
Dakika mbili baadaye (dk 36’) Oscar alifunga goli la nne na msumari wa tano uligongelewa dakika ya 80’ na Andre Schuerrle.
Katika mechi nyingine, Manchester United imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Queens Park Rangers.
Mabao ya Man United yamefungwa na Marouane Fellaini katika dakika ya 58 na James Wilson dakika ya 90 ya mchezo.
Majogoo wa jiji Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aston Villa.
Bao la Fabio Borini katika dakika ya 25’ lilitosha kuwafanya wekundu hao wa Anfield kuwa mbele kwa bao 1-0 ugenini.
Rickie Lambert alitikisha nyavu dakika ya 79 na mpaka dakika 90 zinamalizika, Liverpool walikuwa mbele kwa mabao mawili kwa nunge.
MATOKEO YA MECHI ZOTE HAYA HAPA:
England - Premier LeagueJanuary 17 | |||
---|---|---|---|
FT | 0 - 2 | ||
FT | 2 - 3 | ||
FT | 0 - 1 | ||
FT | 0 - 2 | ||
FT | 0 - 5 | ||
FT | 2 - 1 | ||
20:30 | ? - ? |
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili ambapo mechi ya mjini ni baina ya Manchester City na Arsenal uwanja wa Etihad.
RATIBA YA KESHO
RATIBA YA KESHO
England - Premier LeagueJanuary 18 | |||
---|---|---|---|
16:30 | ? - ? | ||
19:00 | ? - ? |
0 comments:
Post a Comment